Translate

Raisi Obama kuruhusu wakimbizi zaidi kuingia Marekani

Rais Barack Obama, akiwa na kiongozi wa Myanmar's Aung San Suu Kyi nyumbani kwakeYangon, Myanmar mwaka wa 2014
.Rais Barack Obama ametoa mpango wa kuruhusu wakimbizi 110,000 kuingia Marekani mwaka wa 2017 ikiashiria ongezeko la wakimbizi 10,000 zaidi kuliko ilivyopangwa .

Rais Barack Obama ana mpango wa kuruhusu wakimbizi 110,000 kuingia hapa Marekani mnamo mwaka wa 2017 ikiashiria ongezeko la wakimbizi 10,000 zaidi kuliko lengo lake la awali ikiwa ni asilimia 30 zaidi kuliko mwaka huu.

Kulingana na vyombo vya habari waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ametangaza malengo hayo ya kuwapatia wakimbizi makazi Marekani hapo jana wakati wa kikao cha faragha cha kamati za sheria za baraza la seneti na lile la wawakilishi.

Mara ya mwisho kwa Marekani kuweka malengo ya kuwapokea wakimbizi kuwa ya juu kama alivyoweka rais Obama ilikua wakati ni wakati wa utawala wa Rais Bill Clinton 1995 ambapo wakimbizi 112,000 waliruhusiwa kuingia nchini.

Mwaka wa 2015, Marekani iliwakaribisha wakimbizi 70,000 pekee. Kuna uwezekano kuwa Rais Obama atatangaza rasmi mpango huo wa wakimbizi kabla ya kuhudhuria mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Matiafa utakaofanyika
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment