Uchina imeanza kutumia darubini kubwa kabisa ya redio duniani ambayo imesha anza kupata habari kutoka nyota iliyoko masafa yatayochukua zaidi ya miaka elfu moja kwa mwangaza kufika.
Darubini hiyo itawasaidia wanasayansi kuuelewa zaidi ulimwengu na kutafuta viumbe katika sayari nyengine.
Mamia ya wajuzi wa elimu ya nyota na washabiki, wamehudhuria uzinduzi wa darubini hiyo.
Sinia kubwa ya darubini imewekwa kati ya milima kadha katika jimbo la Guizhou, baada ya watu elfu nane kuhamishwa kujenga mtambo huo.
0 comments:
Post a Comment