Translate

Pacha walioshikana kichwani watenganishwa New York



Wavulana wawili pacha ambao walikuwa wameshikana vichwani wametenganishwa na madaktari mjini New York, Marekani.

Jadon na Anias McDonald wa umri wa miezi 13 walifanyiwa upasuaji uliochukua saa 16 katika hospitali ya Montefiore.

Kwa sasa wanafanyiwa matibabu ya kuwezesha mafuvu ya vichwa vyao kukua na kujaza pengo lililoachwa.

Mama yao Nicole McDonald aliandika kwenye Facebook Ijumaa asubuhi jinsi alivyokuwa na furaha lakini pia na "uchungu kuhusu mustakabali wa watoto hao."

Alipakia picha ya Jadon akiwa peke yake kitandani.

"Hata niliwauliza mbona walipanga upya chumba cha kulala kwa sababu haikuwa imeniingia akilini kwamba ningehitaji kitanda cha ziada," Bi McDonald aliandika.

Alisema wasichana hao ni kama wamezaliwa upya.


Madaktari wanasema wavulana hao watalishwa kwa kutumia mifereji kwa kutumia neli (tyubu) kwa wiki moja zaidi

Wavulana hao walizaliwa wakiwa na mishipa ya damu na sehemu za ubongo zilizoshikana, tatizo ambalo hutokea katika kisa kimoja kati ya visa 10 milioni vya kuzaliwa kwa watoto.

Familia ya McDonald ilikuwa imechangisha $100,000 kugharimia upasuaji huo.

Dkt James Goodrich, aliyekuwa amefanya upasuaji sawa kwa watoto wengine wakiwepo pacha kutoka Syria mapema mwaka huu alijiandaa kwa upasuaji huo kwa kutumia mfano wa 3D.
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment