Translate

KIPINDI CHA ZAMARADI MKETEMA CHAFUNGIWA RASMI KWA KUFANYA MAHOJIANO NA SHOGA.



Zamaradi Mketema ni mfanya kazi anayefanya kazi katika kampuni ya clouds media,yeye akijihusisha sana sana kwenye upande wa Televisheni.Huwa ni maarufu sana kwa kurusha kipindi cha Take one ambacho huwa kinajihusha na kuwahoji watu mbalimbali masuala yahusuyo mambo ya kisiasa,kijamii na kiutamaduni.

Mwaka huu kipindi hicho kiliingia doa jeusi baada ya kuendesha kipindi chake kwa kumhoji mtu ambaye anashiriki mapenzi ya jinsia moja yaani "shoga".Kitendo hicho kilileta gumzo kubwa sana kwenye mitandao ya kijamii pamoja na wananchi wote kwa ujumla katika nyanja mbalimbali za habari

Hii ilikuja kwa sababu vitendo hivyo havikubaliwi na jamii yetu ya kitanzania na hivyo kuonekana kana kwamba kuendesha kipindi hicho ni sawa na kuvipalilia vitendo hivyo na kuvipa nafasi au kuvikubali kuwa vinafaa katika jamii yetu.


MAAMUZI YA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA JUU YA KIPINDI HICHO.
Baada ya kamati ya maadili ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania kupata shauri hili juu ya kipindi hiki kurusha matangazo ya ushoga,kamati ilikaa na kutoa uamuzi wake ambao ni kukifungia kipindi hicho kisirushe matangazo yake kwa kipindi cha miezi mitatu pamoja na kutoa onyo kali sana kwa kituo hicho kwa tabia yake hiyo.

Aidha ifahamike kuwa sheria za jamhuri ya muungano wa Tanzania haziruhusu mapenzi na ndoa za jinsia moja na hata uhusiano wa kimapenzi baina ya ndugu.

SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment