BREAKING NEWS::SHIRIKA LA NDEGE LATANGAZA NAULI ZAKE RASMI,NI BAADA YA KUZINDULIWA RASMI MWEZI ULIOPITA.
Shirika la ndege la Jamhuri ya muungano wa Tanzania,limeamua kutangaza safari zake mpya hii ni pamoja na bei zake mpya ambazo ni gharama za nauli za kusafiria kutoka katika mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine.Hii imekuja Rasmi baada ya Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania kuzindua rasmi ndege hizo mbili ambazo zitakuwa zikifanya kazi hizo za usafiri.
Kutoka katika mtandao wao wa twitter shirika hilo limeamua kukaa chini na kutoa mchanganuo wa bei hizo kutoka Daresalaam hadi arusha ambayo ni shilingi 160,000.Huku nauli kutoka Daresalaam hadi mwanza ikibaki kuwa ni hiyo hiyo 160,000
Aidha shirika hilo limesema kwamba bei za ndege hizo ni nauli za kwenda tu na wala si kwenda na kurudi aidha bei za mikoa mingine bado wanafanya mchakato wa namna gani watapeleka safari katika mikoa mingine ya kibiashara kwa ajili ya kuwarahisishia usafiri.
0 comments:
Post a Comment