Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, anahamia mji wa Dodoma zaidi ya miaka 40 tangu mji huo kutangazwa kuwa mji mkuu wa Tanzania.
Anaondoka mji wa Dar es Salaam ulio umbali wa kilomita 450 mashariki.
Hatua hiyo ndiyo ya kwanza ya serikali ya Tanzania kuhamia mji wa Dodoma.
Kwa muda wa miezi miwili iliyopita ofisi za serikali zimekuwa zikihamishwa kwenda mji wa Dodoma.
Rais wa Tanzania John Magufuli alitoa amri mwezi Julai wakati alishika wadhifa wa mwenyekiti wa chama tawala, Chama Cha Mapinduzi.
Shughuli hiyo ya kuhama inatarajiwa kuchukua miaka mitanio na kugharimu dola milioni 500.
Dodoma ulitangazwa kuwa mji mkuu wa Tanzania na rais mwanzilishi Julius Nyerere mwaka 1973.
0 comments:
Post a Comment