Makundi ya waasi nchini Syria
yameonesha kutoridhishwa na kusitishwa kwa mapigano kunakosimamiwa na
Urusi na Marekani ambapo kusitishwa huko kunatarijiwa kuanza Jumatatu
jioni.
Makundi hayo yanatakiwa kusema kama watajiunga kwenye makubaliano hayo ama la.Kuna madai kuwa moja ya kundi la waasi la Ahrar al-Sham watakataa kusitisha mapigano hayo.
Kiongozi wa kikundi kingine cha waasi mjini Alepo amesema kuwa wanakubali kuondoa uhasama na kuruhusu misaada lakini ana wasiwasi na makubaliano.
Mashambuzli ya ndege za Syria na Urusi yameendelea siku ya jumapili katika mji wa Alepo na Idlib.
Zaidi ya watu 100 wameuawa katika mashambulizi yaliotekelezwa siku ya jumamosi.
0 comments:
Post a Comment